Mimi Mars pamoja na kujishughulisha na shughuli za Uanamuziki lakini pia ameonekana kwenye hafla, makongamano kama mshereshaji maarufu kama (MC).
Mimi Mars ambaye ameshawahi kutangaza kwenye moja kati ya vituo vya Televisheni anatuelezea safari yake ya Maisha ya Sanaa ambayo aliianza akiwa na Miaka Nane kwa kuibuka katika kuigiza kwenye Tangazo la Godoro ambalo alilifanya na Marehemu Baba yake.
Kipaji cha Mimi Mars kiliendelea kuchanua akiwa shule baada ya kuonekana kwenye Matamasha mbalimbali yaliyokuwa yanafanyika shuleni.
Kazi yake ya kwanza Mimi Mars ilikuwa ni Mtangazi wa TV lakini baadae akagundua kuwa ana kipaji cha Uimbaji ndipo karama yake nyingine ikaonekana tena ndipo Mwaka 2017 alitoa ngoma yake ya kwanza.
Jina la Mimi Mars lilikuwa kwa kasi sana kupitia Sanaa ya Muziki lakini wakati akiendelea na Muziki aliendelea na Sanaa ya Uigizaji ndipo Muongozaji wa Filamu ajulikanaye kama Lamata Leah ndipo alipomuibua na kufahamika sana kwa jamii kupitia Filamu ya Juakali na sasa anafahamika zaidi na Watanzania kwa jina la Maria.
Pamoja na mambo mengine Mimi Mars pamoja na ndugu zake wamefungua Taasisi inayoitwa Udada Foundation, Taasisi ambayo itakuwa inawasaidia Mabinti kwenye Sekta ya Elimu na Afya lakini inatoa ushauri kwa Mabinti wa Kitanzania.
Mimi Mars anaeleza lengo na nia ya kuanzishwa kwa Udada Foundation lengo likiwa ni kuimarisha tamadanu za Kitanzania kwa Mabinti wa Kitanzania. hadi sasa taasisi hiyo imeshagawa Umeme wa Jua mkoani Arusha lakini pia imeshasambaza Taulo za Kike kwa shule mbalimbali zilizopo Tanzania.