Mauritania: Huduma za intaneti zakatika vurugu za matokeo ya uchaguzi zikitawala

Mauritania: Huduma za intaneti zakatika vurugu za matokeo ya uchaguzi zikitawala

Mgombea wa upinzani Biram Ould Dah Abeid amegoma kukubali matokeo ya uchaguzi na kuyaita "mapinduzi ya uchaguzi."
Rais wa Mauritania Mohamed Ould Ghazouani ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa Rais kwa kupata asilimia 56.12 ya kura. Picha/Reuters

Huduma za intaneti zilishitishwa kwa maeneo mengi nchini Mauritania siku ya Jumanne, ikiwemo kwenye mji mkuu wa Nouakchott, kufuatia vurugu kubwa za kupinga matokeo ya uchaguzi.

Kulingana na mashuhuda, huduma za intaneti na simu zilikatika katika maeneo ya Mauritania.

Mamlaka za mawasilino za Mauritania hazikutoa kauli yoyote kufuatia hali hiyo.

Siku ya Jumatatu, maeneo mengi ya Mauritania, ikiwemo Nouakchott, imeshuhudia wafuasi wa Biram Ould Dah Abeid, walindamana kupinga matokeo hayo.

Mwanasiasa huyo, ameyaita matokeo hayo kama "mapinduzi ya uchaguzi."

Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo, siku ya Jumatatu, umesema kuwa Rais aliye madarakani, Mohamed Ould Ghazouani ameshinda uchaguzi huo kwa asilimia 56.12 ya kura zote, huku Biram Ould Dah Abeid akiwa nafasi ya pili kwa asilimia 22.10.

Siku ya Jumamosi, wananchi wa Mauritania walipiga kura kumchagua kiongozi wao, kati ya wagombea saba.

Nchi hiyo, inayopatikana kaskazini mwa Afrika imeshuhudia matukio kadhaa ya mapinduzi, kuanzia mwaka 1978, 2008 na 2019..

TRT Afrika