Mashambulio yaliyoanza muda mfupi kabla ya saa sita usiku, yameendelea mpaka siku ya Krismasi. / Picha: AA

Shambulio la anga katika kambi ya wakimbizi ya Al Maghazi katikati mwa Gaza limeua angalau watu 70, msemaji wa Wizara ya Afya katika eneo hilo amesema.

Ashraf Al Qudra amesema kinachotokea katika kambi ya Maghazi ni "mauaji ya halaiki" yanayofanywa katika eneo la makazi ya watu wengi.

Ameongeza kwamba, idadi ya vifo inaweza kuongezeka, kutokana na idadi kubwa ya wakazi waliopo katika eneo hilo.

'Nyoyo yetu ziko Bethlehem': Papa Francis

Papa Francis ameitisha amani huku akiongoza misa ya Mkesha wa Krismasi kwenye kanisa kuu la St. Peter's Basilica, Vatican huku mapigano ya Israeli dhidi ya Gaza yakiendelea kupamba moto.

"Usiku wa leo, nyoyo zetu ziko Bethlehem, ambapo amani inakataliwa na fikra za vita,” amewaambia waumini takriban 6,500."

TRT World