Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arusha nchini Tanzania./Picha: TRT Afrika

Jumuiya ya Afrika Mashariki imezidi kusogeza mbele matumaini ya kupata sarafu ya pamoja.

Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo (EAC) Veronica Mueni Nduva, amesisitiza kuwa muundo huo wa kisiasa unaounganisha nchi nane utafikia hatua ya kuwa na sarafu moja mwaka 2031 na sio 2024 kama ilivyokuwa hao awali.

“Mpango wa kuwa na sarafu moja ulikuwa ufikiwe mwaka 2024 kulingana na mkakati uliowekwa. Hata hivyo, haukuweza kutekelezwa mpaka 2031,” amesema Nduva.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Veronica Mueni Nduva./Picha:

Nduva amesema kuwa baadhi ya vipengele ndani ya mkakati na safari ya kufikia sarafu ya pamoja vimetekelezwa, licha ya mgawanyiko mkubwa ulioko kati ya nchi wanachama.

Vipengele hivyo, ni vile vinayohusisha michakato ya kisheria ya kuanzisha umoja wa kifedha.

Kwa mujibu wa EAC, umoja wa Fedha wa Jumuiya hiyo uliosainiwa Novemba 30, 2013 unalenga kuunganisha sarafu za nchi wanachama ili kuwa moja.

Pia, inaelezwa kuwa ucheleweshwaji wa utekelezaji wa itifaki hiyo unaathiri manufaa yaliyotarajiwa, ikiwamo kurahisisha muamala ya kifedha na kuondoa changamoto ya ubadilishaji wa fedha mipakani.

TRT Afrika