Zaidi ya watu milioni 6 wa Sudan wananing'inia kwa uzi kutumbukia katika baa la njaa, yameonya mashirika ya misaada katika taarifa.
Mashirika hayo pia yametoa taswira ya kutisha kuwa zaidi ya watoto milioni 14 wanahitaji msaada wa dharura huku mamilioni wengine wakikimbia nchi kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama.
Taarifa hiyo iliyo iliyotiwa saini na mashirika 14 yakiwemo ya Umoja wa Mataifa, yameitisha mabadiliko ya mara moja kwa namna suala la Sudan linashughulikiwa.
''Ni wakati wa kuwajibika. Tunatoa wito wa kukomeshwa mara moja kwa uhasama.'' imesema taarifa hiyo. ''Watu wa Sudan wanahitaji amani na upatikanaji wa usawa wa misaada ya kibinadamu.'' iliendelea kusema.
Mashirika hayo yalisisitiza masuala matatu, ikiwemo upandewa wa waathiriwa wa mapigano hayo, ikiazimia kuendelea kuwahudumia na kuwatia moyo kutokata tamaa.
''Kwa wale wanaopigana, tunawahimiza kusitisha mara moja. Tunataka kulindwa raia na kwa kuondolewa vikwazo vya urasimu, ili kutuwezesha kufikisha misaada kwa wanaohitaji.'' Ilisem ataarifa.
Jamii ya kimataifa iliombwa kutoendelea kusubiri, na kuchukua hatua zozote ziwezekanazo kurudisha amani na utulivu ndani ya Sudan.
Agosti 15 iliadhimisha miezi minne tangu mapigano kuzuka ndani ya Sudan kulingana na Umoja wa Mataifa,
Maelfu ya watu wameuawa, na wengine kuachwa bila makazi. UN pia imeshutumu maovu yanayotokea nchini humo ikiwemo Ubakaji, Uporaji na kushambuliwa wanawake na watoto, ambao unachunguzwa kama uhalifu wa kivita.