Mashauriano ya Sudan na Marekani yalihitimishwa bila kuafikiana iwapo wajumbe wanaowakilisha jeshi au serikali watashiriki katika mazungumzo ya amani huko Geneva Agosti 14, mkuu wa ujumbe wa Sudan alisema Jumapili.
Ujumbe kutoka serikali ya Sudan ulisafiri hadi Jeddah nchini Saudi Arabia siku ya Ijumaa ili kushauriana na Marekani kuhusu mwaliko wake wa mazungumzo ya kumaliza vita vya miezi 15 kati ya jeshi na wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF).
Mazungumzo ya Geneva, ambayo RSF imekubali kuhudhuria, yatakuwa jaribio la kwanza kubwa katika miezi kadhaa kupata upatanishi kati ya pande mbili zinazozozana nchini Sudan.
Reuters