Wamiliki wa mikokoteni wa Chad husafirisha mali za watu wa Sudan waliokimbia mzozo katika eneo la Darfur nchini Sudan, wakati wakivuka mpaka kati ya Sudan na Chad huko Adre, Chad Agosti 4, 2023. Picha : REUTERS

Eneo la Darfur Magharibi linatishiwa kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kufuatia mapigano yaliyozuka mwishoni mwa wiki.

Walioshuhudia wameambia shirika la Reuters kuwa Ghasia zilipamba moto katika mitaa ya Nyala na kwingineko katika jimbo hilo hadi Jumapili.

Ghasia hizo zinahofiwa kusababisha kufufuliwa kwa mashambulizi yaliyolengwa ya kikabila huko Darfur Magharibi, na kusababisha kuhama kwa zaidi ya watu milioni 4 ndani ya Sudan huku na kuvuka mipaka yake hadi Chad, Misri, Sudan Kusini na nchi nyingine.

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka vya kijeshi yamepamba moto mara kwa mara huko Nyala, jiji la pili kwa ukubwa nchini humo na kitovu cha kimkakati cha eneo tete la Darfur.

Mlipuko huo wa hivi punde umedumu kwa siku tatu, huku jeshi na RSF wakirusha mizinga katika vitongoji vya makazi, walioshuhudia waliambia Reuters. Mapigano yameharibu mitambo ya umeme, maji na mawasiliano ya simu.

Takriban watu wanane waliuawa Jumamosi pekee, kulingana na Chama cha Wanasheria wa Darfur, mfuatiliaji wa haki za binadamu wa kitaifa.

Reuters