Maonesho ya Kimataifa ya Utalii (SITE) yakamilika jijini Dar es salaam, nchini Tanzania.

Maonesho ya Kimataifa ya Utalii (SITE) yakamilika jijini Dar es salaam, nchini Tanzania.

Maonesho hayo yanalenga kutangaza fursa za kuwekeza katika sekta ya Utalii nchini Tanzania.
Utalii unachangia asili mia 17 ya pato la taifa Tanznaia /Picha : TRT Afrika

Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Swahili International Tourism Expo (SITE) yanakamilika hii leo jijini Dar es salaam, nchini Tanzania.

Maonesho hayo yanawakutanisha wadau katika soko la utalii la Tanzania kutoka mataifa ya Afrika na nje ya Afrika.

Vile vile, yanalenga kutangaza fursa za kuwekeza katika sekta ya Utalii nchini Tanzania. Hata hivyo, jukwaa hili linatoa nafasi ya kuhamasisha utalii endelevu na jumuishi kwa kulenga shughuli za utalii zinazojali mazingira na kutoa fursa sawa za maendeleo.

Watoa huduma mbalimbali kwenye soko la utalii kama hoteli, Afya, na fedha ni miongoni mwa wadau wakuu katika maonyesho hayo, lakini wafanyabiashara kwenye Utalii ni miongoni mwa wadau walioshiriki maonesho ya SITE mwaka huu.

''Serikali inaweka mkazo katika kufanya shughuli ya utalii kuwa endelevu na jumuishi ili kuongeza tija ya sekta hiyo inayochangia asilimia 17 ya pato la taifa,'' alisema Angela Kairuki, waziri wa maliasili na utalii wa Tanzania, wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo.

Maonesho hayo maarufu kwa jina la SITE yanayoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania yanafanyika kwa mara ya saba sasa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2014 yakihusisha waoneshaji takriban 150 na wanunuzi kutoka Mataifa 70 duniani.

TRT Afrika