Wanajeshi wa nchini Malawi wanaendelea kuitafuta ndege iliyokuwa imembeba Makamu wa Rais wa nchi hiyo iliyopoteza mawasilino na rada siku ya Jumatatu, Rais Lazarus Chakwera amesema.
Hata hivyo, idara ya udhibiti wa anga iliitaka ndege hiyo kusitisha zoezi la kutua na kugeuza kutokana na hali mbaya ya hewa, alisema Rais Chakwera katika hutoba yake kwa taifa.
Kitengo hicho kilipoteza mawasiliano na ndege hiyo na ikatoweka kwenye rada muda mfupi baadaye, alisema.
“Najua hili ni jambo la kushtua kidogo. Najua sote tuna uoga na wasiwasi.
Hata mimi nina hofu,” alisema Chakwera . Lakini naomba niwahakikishie kuwa tunafanya kila jitihad akuitafuta ndege hiyo kukiwa na matumaini ya kuwapata manusura.”
Mzuzu ni mji wa tatu kwa ukubwa nchini Malawi. Unapatikana katika eneo lenye milima na misitu mingi.
Kiongozi huyo aliahidi kuendeleza msako wa ndege hiyo hadi usiku na kuongeza kuwa mamlaka zilitumia minara ya mawasiliano kuitafuta ndege hiyo, ndani ya kilomita 10 kutoka eneo la mashamba.
Kulingana na Rais Chakwera, zoezi hilo la utafutaji linaongozwa na Jeshi la Ulinzi la nchini Malawi.
“Nimetoa maagizo kuwa utafutaji uendelee hadi ndege ipatikane,” alisema Chakwera.
Chakwera aliongeza kuwa Marekani, Uingereza na Israeli zimejitolea kusaidia zoezi la utafutaji wa ndege hiyo kutokana na teknolojia zao za kisasa, na kuonesha matumaini ya kupatikana kwa ndege hiyo.
Chakwera alisema Dzimbiri, aliyekuwa mke wa zamani wa Rais wa zamani Bakili Muluzi, alikuwa ni mmoja wa abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo, wakielekea kuhudhuria mazishi ya waziri wa zamani.