Makamu wa Rais wa Afrika Kusini 'aendelea vizuri' baada ya kudondoka jukwaani

Makamu wa Rais wa Afrika Kusini 'aendelea vizuri' baada ya kudondoka jukwaani

Paul Mashatile alidondoka jukwaani wakati wa akihutubia katika hafla ya kumsimika kiongozi wa jadi.
Inaelezwa kuwa Makamu wa Rais wa Afrika Kusini Paul Mashatile alizidiwa na hali ya joto wakati wa kutoa hutoba hiyo./Picha: AFP

Afya ya Makamu wa Rais wa Afrika Kusini Paul Mashatile inazidi kuimarika hata baada ya kudondoka jukwaani wakati anasoma risala siku ya Jumamosi mchana, mwakilishi wa Jimbo la Limpopo aliliambia Shirika la Habari la Afrika Kusini (SABC).

Mashatile alikutwa na kadhia hiyo wakati akisoma risala katika hafla ya kumsimika kiongozi wa jadi katika eneo la Tzaneen, lililopo katika jimbo la Limpopo, kilomita 412 kaskazini mashariki mwa limesema Shirika la SABC.

Mwakilishi wa jimbo la Limpopo ambaye pia ni daktari Phophi Ramathuba, ameiambia SABC kuwa hali ya Mashatile ilizidi kuimarika, licha ya kuzidiwa na joto wakati akielekea kumaliza kusoma risala yake.

"Makamu wa Rais anaendelea vizuri, yuko chini ya uangalizi wa timu ya madaktari wake. Nilikuwa nao, yuko sawa kwa sasa, hakuna haja ya kuhofia chochote," alisema Ramathuba.

TRT Afrika