Mahakama ya Juu ya Kenya Jumanne ilikataa ombi la mawakili wa naibu rais la kusimamisha bunge la seneti kujadili hoja ya kumwondoa madarakani baada ya bunge kupiga kura ya kumuondoa madarakani wiki jana.
Jaji Chacha Mwita aliamua kwamba bunge litaruhusiwa kuendelea na mamlaka yake ya kikatiba na mahakama "haitaingilia."
Hoja ya kutimuliwa kwa Naibu Rais Rigathi Gachagua iliidhinishwa kwa kura 281-44 bungeni wiki jana na kutumwa kwa bunge la seneti ambalo litaanza kusikilizwa Jumatano.
Gachagua anakabiliwa na mashtaka dhidi ya ufisadi na makosa mengine, ikiwa ni pamoja na madai kwamba aliunga mkono maandamano ya kuipinga serikali mwezi Juni. Gachagua anakanusha mashtaka yote dhidi yake.
Maombi sita
Chini ya Katiba ya Kenya, kuondolewa madarakani ni moja kwa moja ikiwa kutaidhinishwa na mabunge yote mawili, ingawa Gachagua anaweza kupinga hatua hiyo mahakamani - jambo ambalo amesema atafanya.
Jaji mkuu mnamo Jumatatu aliidhinisha jopo la majaji watatu kusikiliza maombi sita yaliyowasilishwa dhidi ya mchakato wa kumuondoa madarakani.
Mjadala unaohusu hatima yake umeenea zaidi ya bunge - wafuasi na wapinzani wa hoja hiyo walikabiliana wiki iliyopita katika majukwaa ya hadhara baada ya muungano unaotawala kuleta hoja hiyo bungeni.
Rais William Ruto bado hajazungumza hadharani kuhusu kuondolewa kwake madarakani, lakini amenukuliwa katika siku za awali za urais akisema hatamdhalilisha hadharani naibu wake, akigusia uhusiano mbaya aliokuwa nao na mtangulizi wake, Uhuru Kenyatta, wakati wa awamu ya pili madarakani.
Theluthi mbili ya wengi
Bunge la seneti linahitaji kura ya thuluthi mbili ili kuidhinisha hoja ya kumtimua.
Iwapo itaidhinishwa, itakuwa mara ya kwanza kwa naibu rais aliyeko madarakani kushtakiwa nchini Kenya