Mafuriko na maporomoko ya ardhi katika eneo la pwani ya Kenya yamesababisha ucheleweshaji wa kupeleka mizigo na kutoka katika mji wa bandari wa Mombasa, kampuni ya reli inayomilikiwa na serikali ilisema Jumamosi.
Mvua kubwa iliyofuatwa na mafuriko imesababisha miji mingi ya Afrika Mashariki kufurika maji na kusababisha mamia ya maelfu ya watu kukosa makazi.
Nchini Kenya, idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko inafikia angalau 46, na inatarajiwa kuongezeka.
Mafuriko hayo kwenye njia ya reli kati ya mji mkuu Nairobi na Mombasa yamelazimu shirika la reli la Kenya kufunga huduma zote za mizigo, ilisema katika taarifa yake. Reli hiyo pia hutumika kusafirisha mizigo katika nchi zikiwemo Rwanda, Uganda na Sudan Kusini.
Hata hivyo taarifa hiyo ya shirika la reli ilisema kuwa huduma ya usafiri wa abiria utaendelea bado japo kwa kupunguzwa idadi.
Mvua kubwa inayoendelea kunyesha imesababisha uharibifu mkubwa katikamaeneomengi ya Afrika Mashariki ikiwemo Somalia, Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda.
Awali kulikuwa na taarifa za tahadhari zilizotolewa na baadhi iya serikali na taasisi za kimataifa za kufuatili atabia nchi, kwamba kun auwezekanomkubwa wa kutokea El Nino, janga linalosababisha mvua ya mafuriko na maporomoko ya ardhi, ambalo kawaida hufuatia janga la ukame wa muda mrefu.