Burundi Watoto wakikimbia / Photo: AP

Maelfu ya familia wamekosa makazi kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini humo.

Simeon Butoyi, mmoja wa maafisa katika eneo lililokumbwa na mafuriko la Mutimbuzi Magharibi mwa nchi, alisikitishwa na athari mbaya ya mafuriko kwa maisha ya raia.

"Familia 4,000 zimehamishwa kutoka kwa makazi yao na kuhamia maeneo mengine kutokana na mafuriko haya," alisema Bw. Butoyi.

"Nyumba za watu wengi sasa zimeharibika, watu hulala usiku katika maeneo ya wazi kwenye mazingira ya baridi," aliongeza Simeon Butoyi.

Watu 800,000 wanaoishi, kanda ya Ziwa Tanganyika ulioko Magharibi mwa nchi, huwa wako hatarini kuathiriwa na mafuriko.

AA