Mamlaka katika ofisi ya Naibu Rais wa Kenya aliyeondolewa Rigathi Gachagua imewaagiza maafisa 108 wa ngazi za juu katika ofisi hiyo kwenda likizo ya lazima kuanzia Jumamosi saa sita mchana, wakiwemo baadhi ya washauri wakuu wa Naibu Rais huyo.
Katika barua ya ndani ya usimamizi, mamlaka hiyo ilisema pia imesitisha mikataba yote ya wafanyakazi wa kandarasi za muda.
"Maafisa wote walioorodheshwa katika Vikundi vya Kazi T na U wanaagizwa kuenda likizo ya lazima mara moja," ilisoma risala iliyoandikwa na Patrick Mwangi, Katibu Mkuu Tawala katika Ofisi ya Naibu Rais.
Risala hiyo ambayo pia nakala yake ilitumwa kwa mkuu wa utumishi wa umma wa ikulu, ilisema kuwa agizo hilo linatekelezeka kuanzia saa sita mchana Jumamosi.
Hii inakuja wakati Rais William Ruto anakabiliwa na changa moto nyingine ya kumteua atakaye shikilia wadhifa wa Naibu Rais, huku kesi za kupinga chaguo lake zikiwasilishwa mahakamani.
Mahakama iliagiza Ijumaa kusitishwa utekelezwaji wa kumoundoa Gachagua kutoka ofisini pamoja na mchakato wa kumteua mrithi wake kadi Alhamisi ijayo 24, ambapo kesi hiyo itaamuliwa mbele ya jopo l amajaji watatu.