Mining

Katika juhudi za kurahisisha sekta ya madini yenye faida na kuibua uwezo wake kamili kupitia Sheria ya Madini iliyopitishwa hivi majuzi ya 2016, serikali ya Kenya inajaribu kurejesha imani ya wawekezaji wa kigeni katika sekta ya madini.

Kenya imekuwa ikifanya kazi kwa kasi kuelekea kuundwa kwa sheria ya kisasa ya uchimbaji madini ambayo italeta uwiano unaofaa kati ya maslahi ya wawekezaji, maslahi ya umma, na wajibu wa kifedha kwa wamiliki wa haki za madini

Akiwaongoza wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Idara ya Mazingira, Misitu, na Madini ya Bunge katika ziara ya Eneo la Msingi la Mgodi wa Titanium Kwale,Katibu Mkuu wa Madini wa Kenya, Elijah Mwangi, alisema sheria hii mpya ya madini ilichukua nafasi ya Sheria ya Madini Sura. 306 ya mwaka wa 1940

Hatua hii inachukuliwa wakati ambapo wawekezaji wa kigeni wanazidi kuchoshwa na sheria na sera zilizokua hapo awali zimeathiri vibaya shughuli zao za biashara.

‘Wasiwasi, kutokuelewana, na kesi za kisheria ndio ilikua utaratibu wa Sheria ya Madini Sura ya mwaka1940 na zimeisumbua sekta hii kwa miaka mingi. Hayo sasa ni mambo ya kale’ alisema Katibu

Kutokana na hali hiyo, leseni 65 za utafutaji na uchimbaji madini zimewai kufutwa hapo awali, na zuio la kudumu la utoaji wa leseni mpya kuwekwa mwaka 2013.

Jamii na serikali za kitaifa na kaunti lazima kila moja ipokee asilimia 70-20-10 ya mraba inayolipwa na mwenye haki za madini.

Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi, Hazina ya Kitaifa inapokea kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa uchimbaji wa madini. Alidokeza kuwa idara ya hazina ya serikali hivi karibuni italipa mabilioni ya shilingi za mrabaha wa madini kwa kaunti na vijiji ambako uchimbaji madini unafanyika.

Dkt. Melba Wasunna, meneja wa masuala ya nje wa Base Titanium aliyekuwepo pia katika mkutano huo, akiashiria furaha yake alisema kuwa kampuni ya uchimbaji madini ya Australia yenye makao yake makuu katika kaunti ya Kwale inatumai serikali itapunguza marufuku ya vibali vipya vya uchimbaji madini ili iweze kufanya uchunguzi na uwezekano wa kupanua shughuli zake nchini.

Kurahisishwa kwa Sheria ya Uchimbaji Madini ya 2016 ilihitajika sana kwa sababu Kenya ilikosa mfumo mwafaka wa uchunguzi wa madini na maendeleo ya sekta, haingefika kwa wakati bora zaidi.

TRT Afrika