Haiti imekuwa ikikumbwa na ghasia za magenge, hasa katika mji mkuu Port-au-Prince ambako maeneo makubwa yanadhibitiwa na magenge. / Picha: Reuters

Kikosi cha Kenya kitaondoka kuelekea Haiti Juni 25 kuongoza ujumbe wa kimataifa unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kukabiliana na ghasia za magenge katika nchi hiyo ya Caribbean, vyanzo vya serikali na polisi viliiambia AFP Jumapili.

"Maandalizi yamepangwa kwa timu hiyo kuondoka kuelekea Haiti siku ya Jumanne," afisa mkuu wa polisi alisema kwa sharti la kutotajwa jina.

Chanzo cha pili cha wizara ya mambo ya ndani kilithibitisha tarehe ya kuondoka.

Kenya imetoa maafisa 1,000 wa polisi kwa misheni ya kimataifa ya usalama nchini Haiti.

Taifa hilo la Caribbean limekumbwa na ghasia za magenge, hasa katika mji mkuu Port-au-Prince ambako maeneo makubwa yanadhibitiwa na magenge.

Hatua ya Kutumwa polisi wa Kenya huko kumegawanya taifa la Afrika Mashariki tangu mwanzo. Ilizua mjadala mkali bungeni na miongoni mwa maafisa katika angalau wizara mbili kuhusu iwapo Kenya inafaa kuongoza misheni hiyo.

Wanaharakati wa haki pia wamekuwa wkaipinga wakati wingine hadi mahakamani kujaribu kuzuia kutumwa kikosi hicho kikidai kuwa hakujakuwana mafunzo ya kutosha kwa maafisa wa Kenya kuweza kukabiliana na hali hatari iliyoko Haiti, madai ambayo maafisa wakuu wa polisi wa Kenya wamepuuzilia mbali.

Kikosi hicho kitafadhiliwa kwa kiasi kikubwa na Serikali ya Marekani ambayo haitowatuma maafisa wake bali itatoa ufadhili na vifaa chini ya muongozo wa Umoja wa mataifa.

TRT Afrika