Jengo jipya na la kisasa la Bunge limezinduliwa nchini humo na Rais William Ruto.
Jengo hilo linatarajiwa kuwapa watunga sera hao wa bunge la kitaifa na maseneta nafasi ya kutosha ya kufanya kazi kwa ufanisi.
Likiwa na ofisi 331 za Wabunge na Maseneta zinazopatikana kuanzia ghorofa ya 6 hadi ya 22, jengo hilo linaakisi nembo ya ngao ya Bunge.
Ghorofa ya kwanza ya jengo hilo ina Maktaba ya kisasa yenye kumbukumbu zote za bunge kuanzia 1910.
Pia, lina maegesho 350 ya magari na ukumbi maalumu wa mazoezi.
Jengo hilo, lenye jumla ya ghorofa 26 lina huduma muhimu kama vile majiko na mikahawa kwa ajili ya maandalizi ya chakula cha wabunge na wahudumu wengine.
Jengo hili jipya limeleta afueni kwa Wabunge na wafanyakazi kutokana na uhaba wa nafasi hapo awali.