Shirika la habari la Reuters liliripoti tarehe 24 na 25 mwezi Mei mwaka huu kwamba kuanzia mwaka wa 2019, wavamizi wa Kichina walilenga mitandao ya wizara na taasisi muhimu za serikali ya Kenya.
Wizara ya usalama wa ndani na utawala wa kitaifa nchini Kenya umekanusha madai haya.
"Sehemu kubwa ya mtandao muhimu wa Kenya umeimarishwa kutoka Uchina , taarifa imeongezea, " na hivyo kama nchi ya asili ingetamani kupenyeza mifumo kama hiyo ambayo imesaidia kusakinisha, haingehitaji kutumia wahusika wengine."
Ripoti hiyo ilidai udukuzi huo unajumuisha kampeni ya miaka mitatu ambayo ililenga wizara nane za Kenya na idara za serikali.
"Ripoti hiyo inapaswa kutazamwa kama propaganda iliyofadhiliwa," imesema katika taarifa iliyotolewa na Raymond Omollo katibu mkuu wa wizara hiyo.
Wizara hiyo inasema serikali itaendelea kuimarisha usalama na uthabiti wa mifumo yake yote muhimu na miundombinu husika. Hii inasema inafanywa kupitia sera ya usalama wa taifa.