Rais wa Kenya ameomba radhi hadharani kutokana na vifo vinavyohusishwa na ibada ya siku ya maangamizi ambayo imedai waathiriwa 201 huku miili zaidi ikiendelea kuchimbwa kwenye msitu katika eneo la pwani.
Zaidi ya watu 600 wanaodhaniwa kuwa washiriki wa madhehebu ya Kikristo bado hawajulikani walipo.
"Ninachukua jukumu kwamba, kama rais, hivi (vifo) havipaswi kutokea. Kwa hilo, nasema kweli, samahani," Rais William Ruto alisema Jumapili usiku katika mahojiano na televisheni na vyombo vya habari vya Kenya.
Miili hiyo inaaminika kuwa ya wafuasi wa mhubiri wa Kikristo wa eneo hilo, Paul Mackenzie,, anayedaiwa kuwaagiza wafe njaa ili wapate wokovu.
Taarifa zaidi zinasema watoto walilengwa kwanza, na wanawake na wanaume kufuata, kulingana na ripoti.
Mackenzie alikamatwa mwezi uliopita na bado yuko chini ya ulinzi wa polisi pamoja na mkewe. Mazishi ya halaiki yalipatikana katika ardhi yake yenye msitu mkubwa katika kaunti ya Kilifi na polisi walisema anaweza kukabiliwa na mashtaka yanayohusiana na ugaidi.
Upungufu wa polisi, shirika la kijasusi na wasimamizi wa eneo hilo ndio waliosababisha kushindwa kuzuia vifo hivyo, rais alisema. Aliahidi kutembelea maeneo ya maziko mara uchunguzi utakapokamilika.
“Baadhi ya watu wanao husika na kushindwa kuzuia hili kwa upande wa Serikali watalazimika kuwajibiswa,” alisema.
Tume ya uchunguzi imeundwa kuchunguza jinsi waathiriwa walivyoshawishiwa hadi vifo vyao na ukiukwaji wa haki za binadamu makanisani. Lakini baadhi ya makasisi wameeleza kutoridhishwa kuendeshwa kipolisi katika makanisa.
“Tunataka kuanzisha, (pamoja) na viongozi wa kidini, namna bora wanavyoweza kuafikiana kuhusu utaratibu unao hakikisha wahalifu na walaghai hawatumii fursa ya dini na imani kusababisha madhara,” Rais Ruto alisema.
Wakenya ni jumuiya ya kidini na wahubiri wanaoahidi uponyaji wa miujiza na mafanikio ya kifedha huvutia idadi kubwa ya waumini.