Mradi huo unalenga kupunguza gharama kubwa za usafirishaji wa mizigo na abiria./Picha: Getty   

Serikali ya Uganda imeichagua kampuni ya Yapi Merkezi kutoka Uturuki, kufanikisha ujenzi wa njia ya Mashariki ya treni ya kisasa ya SGR.

Mradi huo ambao, utahusisha njia ya kutoka Malaba kuelekea Kampala, unatarajiwa kutekelezwa kabla ya mwisho wa mwaka 2024.

Mratibu wa mradi huo, Perez Wamburu amethibitisha kuhusika kwa kampuni ya Yapi Merkezi kutoka Uturuki katika ujenzi wa reli hiyo yenye thamani ya mabilioni ya fedha.

“Tuko katika hatua za mwisho za makubaliano na kampuni ya Yapi Merkezi. Tumejadiliana masuala ya gharama za mradi,” amesema Wamburu.

Kulingana na mratibu huyo, chaguo la Yapi Merkezi inafuatia kazi nzuri iliyofanya na kampuni hiyo katika ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR nchini Tanzania.

"Tumejiridhisha na kile kilichofanyika nchini Tanzania," ameeleza.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizindua treni ya kisasa ya SGR, mjini Dar es Salaam, Agosti 2, 2024./Picha: Ikulu Tanzania

Tanzania ilizindua safari za treni hiyo ya kisasa Agosti 2, 2024, huku kampuni hiyo kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, Morogoro hadi Makutupora, Makutupora hadi Tabora na Tabora hadi Isaka.

TRT Afrika