Ndege ikiruka huku moshi ukiongezeka ukizua moto katika uwanja wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenya (JKIA) jijini Nairobi. / Picha: Reuters

Moto mkubwa ulizuka siku ya Ijumaa katika eneo la nyasi karibu na barabara za Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), uwanja wa ndege wenye shughuli nyingi zaidi Afrika Mashariki.

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya lilithibitisha kuwa lilikuwa likifanya kazi na timu za kukabiliana na dharura ili kudhibiti moto huo.

"Vikundi vya kukabiliana na dharura viko kwenye eneo , wakipambana na moto wa nyasi ndani ya JKIA. Juhudi zinaendelea kudhibiti moto huo na kuzuia kuenea zaidi,” shirika hilo lilisema kwenye taarifa.

Video zilizochapishwa mtandaoni na wasafiri Ijumaa zilionyesha moto huo ukisambaa katika eneo kubwa na kuwaka karibu na njia ya kurukia ndege.

Shughuli za usafiri hazijaathirika

Hata hivyo Mamlaka ya usimamaizi wa viwanja vya ndege Kenya, KAA ilisema kuwa hakukuwa na atahri yoyote kwa shughuli za usafiri katik auwnaja huo.

Moto huo, ambao ulienea kwa hatari karibu na miundombinu muhimu ya uwanja wa ndege, ulizua wasiwasi juu ya uwezekano wa usumbufu. Walakini, mamlaka iliwahakikishia umma kuwa shughuli za ndege zinaendelea kama kawaida.

"Timu iliyoratibiwa ya kukabiliana na hali hiyo, ikiwa ni pamoja na Huduma ya Uokoaji na Kupambana na Moto katika Uwanja wa Ndege wa KAA, Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF), na Kitengo cha Zimamoto cha Kaunti ya Nairobi, kinafanya kazi kwa bidii kudhibiti hali hiyo," KAA ilisema katika taarifa.

"Shughuli zote za uwanja wa ndege, ikiwa ni pamoja na ratiba za ndege, usindikaji wa abiria, na kushughulikia mizigo, bado inafanya kazi kikamilifu na haijaathiriwa," taarifa hiyo iliongeza.

Matukio ya awali ya moto JKIA

Abiria na wafanyakazi wa uwanja wa ndege walishauriwa kuwa macho huku maafisa wakifuatilia hali hiyo.

Hili si tukio la kwanza kuhusiana na moto katika JKIA.

Mnamo 2013, moto mkubwa uliharibu terminal ya kimataifa ya kuwasili, na kusababisha usumbufu mkubwa.

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) ndio uwanja wa ndege wenye shughuli nyingi zaidi Afrika Mashariki na miongoni mwa viwanja 10 bora vya ndege barani Afrika, kulingana na Baraza la Kimataifa la Viwanja vya Ndege (ACI). Inatumika kama kitovu kikuu cha kikanda cha trafiki ya abiria na mizigo, inayounganisha Afrika na maeneo makuu ya kimataifa.

TRT Afrika