Rais wa Marekani Joe Biden amemualika rasmi mwenzake wa Kenya William Ruto kwa ziara ya kiserikali iliyoratibiwa kufanyika Mei 23 ili kuongeza uhusiano na mshirika wake muhimu wa Afrika Mashariki, Ikulu ya White House ilisema ijumaa.
Ziara hiyo ni katika maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Kenya.
Rais William Ruto, ambaye ataandamana na mkewe Rachel, amealikwa rasmi Ikulu ya White House kwenye ziara ya tarehe 23 Mei kama hatua ya kukuza uhusiano, Ikulu ya White House ilisema Ijumaa.
"Ziara ijayo itaadhimisha miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Kenya na itasherehekea ushirikiano utakaowaunganisha watu wa Marekani na Kenya," Msemaji, Karine Jean-Pierre alisema.
Kwa muda mrefu, Marekani, imekuwa ikiiona Kenya kama mshirika muhimu barani Afrika na katika miaka ya hivi karibuni, imesifu kujitolea kwake kwa demokrasia.
Jean-Pierre ameongeza kuwa " uongozi wa Afrika ni muhimu katika kushughulikia vipaumbele vya kimataifa."