Kampuni ya kusambaza Umeme Nigeria ya Abuja (AEDC), imeipa ikulu ya Nigeria notisi ya hadi tarehe 28 Februari, la kulipa limbikizo la deni la umeme la sivyo itakatiza usambazaji wa huduma hiyo muhimu.
Ifikapo Februari 28, 2024, tutaanza kukatiza huduma zetu kwao hadi watakapotimiza majukumu yao kwetu kwa kulipa deni lao,” AEDC imesema.
Aidha, kampuni ya Umeme AEDC, imetoa 'ilani ya siku 10' kwa ikulu, wizara, idara, na jumla la mashirika 86, kulipa deni la zaidi ya Naira bilioni 47 (dola 295,504,55). Deni hilo ni la tangu Disemba 2023.
Hata hivyo, ikulu imesema inadaiwa N342, 352, 217 ($215,248) na Kampuni hiyo na wala sio N923 milioni ($ 580,320) kama inavyodaiwa na kampuni hiyo.
Kupitia taarifa iliyosainiwa na Mshauri Maalum wa Rais wa Habari na Mkakati, Bayo Onanuga, Jumanne, Rais Tinubu alitoa amri,"Utatuzi wa haraka wa madeni ya umeme... baada ya pande zote kufanya marekebisho na kuridhishwa.’’
"Mkuu wa ofisi ya Rais, Femi Gbajabiamila, amehakikisha kwamba deni hilo litalipwa kwa AEDC kabla ya wiki hii kukamilika," taarifa hiyo ilisema.