OIdara ya afya ya umma imetoa wito wa watu kuwa makini kuepuka maji machafu ili kuzuia kusambaa kwa kipindupindu / Picha: Reuters

Taarifa kutoka kwa Idara ya afya ya umma ya mkoa wa Gauteng inasema kuwa kufikia Jumatatu, watu 17 wamethibitishwa kufa kutokana na ugonjwa huo huku wengine 67 wakiwa wamelazwa hospitalini kutokana na maambukizi ya tumbo.

Jumla ya watu 29 wamethibitishwa kuambukizwa kipindupindu na wamelazwa katika hospitali mbali mbali katika kitongoji cha Tshwane.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, idara ya afya ya umma ya Gauteng imewaimiza watu kuwa makini katika usafi wa chakula na maji wanayo kunywa ili kuepuka maambukizi.

Pia imewataka wale walio na dalili za Kutapika, kuumwa na tumbo, na kuharisha kufika zahanati za karibu nao ili kupokea matibabu ya dharura.

Kipindupindu kimetajwa na shirika la afya duniani kuwa ni miongoni mwa magonjwa hatari zaidi yanayoweza kuua kwa chini ya saa 48 usipo tibiwa ipasavyo.

TRT Afrika