Jeshi lachukua mamlaka nchini Gabon siku 3 baada ya uchaguzi / Picha: Reuters

"Nchi yetu nzuri, Gabon, daima imekuwa kimbilio la amani.

"Leo hii, nchi inapitia matatizo makubwa ya kitaasisi, kisiasa, kiuchumi na kijamii.

“Kwa hivyo tunalazimika kukiri kwamba tume ya uchaguzi mkuu wa tarehe 26 Agosti 2023 haikutimiza masharti ya kufanikisha kura ya uwazi, ya kuaminika na jumuishi kiasi kilichotarajiwa na raia wa Gabon.

"Kilichoongezwa kwa hili ni utawala usio na uwajibikaji na usiotabirika, unaosababisha kuendelea kuzorota kwa uwiano wa kijamii, na hatari ya kuingiza nchi katika machafuko."

"Leo, tarehe 30 Agosti 2023, sisi - vikosi vya ulinzi na usalama, tumekusanyika kama Kamati ya Mpito na Urejeshaji wa Taasisi (CTRI) kwa niaba ya watu wa Gabon na kama wadhamini wa ulinzi wa taasisi - tumeamua kulinda amani. kwa kukomesha utawala uliopo. "

“Kufikia hapa, uchaguzi mkuu wa tarehe 26 Agosti 2023 na matokeo yake yaliyokarabatiwa, yamefutiliwa mbali."

"Mipaka imefungwa hadi matangazo mengine."

“Taasisi zote za Jamhuri zimevunjwa: serikali, Seneti, Bunge la Kitaifa, Mahakama ya Katiba, Baraza la Uchumi, Kijamii na Mazingira na Kituo cha Uchaguzi cha Gabon. "

"Tunatoa wito wa amani na utulivu kutoka kwa umma, jamii za nchi ndugu zetu zinazoishi Gabon, na raia wa Gabon wanaoishi nje ya nchi. "

"Watu wa Gabon, hatimaye tuko kwenye njia ya furaha."

"Mungu na roho za baba zetu ibariki Gabon, heshima na uaminifu kwa nchi yetu. "Asante."

AFP