Hafla hiyo ni jitihada za kuleta katika ajenda matatizo mbalimbali ya dunia na migogoro ya kibinadamu yanayoathiri mamilioni ya watu huku ikiibua nguvu ya sinema," Altun amesema. / Picha: Maktaba AA  / Photo: AA Archive

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais wa Uturuki Fahrettin Altun ametoa hotuba katika Hafla ya 'Filamu inayoangazia masulaua ya ya Kibidamamu ijulikanayo 'TRT World Citizen Humanitarian Film Festival' akisisitiza jukumu la dunia kukabiliana na migogoro ya kibinadamu.

"Taarifa na takwimu zilizopo, haijalishi umuhimu wake, hazitoshi kuondoa mateso ya wanaodhulumiwa; badala yake, ni simulizi inayoonekana katika filamu na sanaa yenye nguvu ya kugusa mioyo yetu," amesema siku ya Jumapili.

Altun ametaja umuhimu ya huruma ya kweli, nguvu ya simulizi, na umuhimu wa utatuzi wa kibinadamu katika kutatua changamoto za kikanda na kidunia. Ameongeza kusema kwamba, ni jukumu la kila mmoja katika jumuia ya kimataifa kupambana na wale ambao wanahusika na matendo ya kikatili yanayosababisha mateso kwa watu katika maeneo mbalimbali ya dunia.

"Kinachotugusa sisi kuzungumzia migogoro ya kibinadamu sio tu kupungua kwa majanga, bali ni uwezo wa kuhimiza na maumivu ya kila mmoja aliyeathirika."

"Sherehe ya Filamu ya inayoangazia masuala ya Kibinadamu," iliyoratibiwa na TRT World Citizen, ambayo inafanyakazi "kwa misingi ya ubinadamu" kuongoza na kuacha alama kwa raia duniani, kwa mara nyengine, imeleta pamoja watazamaji na wataalamu katika tasnia mwaka huu.

Filamu hiyo fupi, ambayo imeratibiwa kwa mara ya 5, ina lengo la kuibua mambo ya kibinadamu ya ulimwengu kwa kulenga zaidi katika mada mbalimbali ikiwemo vita, migogoro, majanga, haki za wanawake, uhamiaji, masuala ya hali ya hewa, uharibifu wa mazingira, njaa, ukame, ukosefu wa makazi na umaskini.

'Suala la Israel'

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki Altun ametaka kuwe na mabadiliko ya jinsi mgogoro wa muda mrefu kati ya Israel na Palestine unavyoeleweka. Amesisitiza kwamba, tatizo, mara nyingi linajulikana kama "tatizo la Palestine." badala yake litambulike kama "tatizo la Israel."

"Leo, tuko hapa kutangaza rasmi jina la tatizo hili kwa dunia, ambalo kwa miaka mingi, limekuwa likijulikana kama tatizo la Palestine. 'Jina la tatizo hili ni 'tatizo la Israel." Altun amesema, na kuongeza kwamba, "sio tu Mashariki ya Kati, sio tu kanda yetu, lakini dunia nzima inakabiliwa na jambo hili."

Ameongeza kusema kwamba, wakati Uturuki imechukuwa msimamo thabiti kukabiliana na changamoto, baadhi wamebaki kimya katika mgogoro huu wa kibinadamu, akisisitiza dharura ya ushirikiano wa dunia.

"Baadhi ya nchi zimeshindwa kuonyesha ujasiri wa kukabiliana na hili jambo, pia kulifumbia macho, lakini Uturuki iko mstari wa mbele," amesema.

"Kadri tatizo la Israel linavyozidi kufumbiwa macho, tatizo hilo la kihistoria linalokuwa litaendelea na kuhatarisha ubinadamu baadae."

Altun amegusia umuhimu wa jukumu la simulizi na sanaa kwa kuongeza uelewa na huruma kwa wanaopata taabu na kudhulumiwa.

Amesifu Sherehe za Filamu za 'TRT World Citizen Humanitarian Film Festival' kwa uwezo wake wa kipekee wa kuonyesha matatizo ya dunia na migogoro ya kibinadamu kupitia kioo cha sinema.

Amemalizia hotuba yake kwa kuonyesha matumaini kwamba, sherehe hiyo, kama mwanzo, itachangia amani ya dunia, maendeleo, haki na utulivu na kuwaleta watengeneza filamu na wasimulizi kuongeza athari yake katika kuangazia matatizo ya kibinadamu yaliyopo duniani.

TRT Afrika