Wazazi wanaoomboleza wakibeba mabango  wakati wa mkutano wa wanahabari, wakitaka haki itendeke kwa vifo vya watoto wanaohusishwa na dawa za kikohozi zilizoambukizwa, huko Serekunda, Gambia, Novemba 4, 2022. / Picha: Reuters

Gambia itafanya kuwa ni lazima kwa bidhaa zote za dawa kutoka India kukaguliwa na kupimwa kabla ya kusafirishwa kuanzia Julai 1, kulingana na hati za serikali ya Gambia zilizopitiwa na Reuters, vikwazo vya kwanza vinavyojulikana kwa mauzo ya nje ya kitaifa kufuatia vifo vya watoto kadhaa wanaohusishwa na Dawa za kikohozi kutoka India.

Sheria hiyo mpya inaangazia jinsi serikali zinavyo tathmini upya utegemezi wao kwenye tasnia ya dawa ya India yenye thamani ya dola bilioni 42 tangu uchafuzi huo ulipodhihirika mwaka jana.

Viwanda vya dawa vya India hutoa karibu nusu ya dawa zinazotumika barani Afrika.

Mnamo Aprili, serikali ya India ilisema maafisa wake walikuwa na mikutano barani Afrika ili kuhakikisha uuzaji wake wa dawa hautaathirika baada ya watoto wasiopungua 70 kufariki nchini Gambia baada ya kumeza dawa ya kikohozi mwaka jana.

Hatua ya hivi punde ya Gambia ni "kudhibiti dawa duni na bandia zinazoingia nchini", mkurugenzi mtendaji wa wakala wake wa kudhibiti madawa (MCA), Markieu Janneh Kaira, aliandika 15 Juni, katika barua kwa mdhibiti mkuu wa dawa za India, Rajeev Singh.

Barua hiyo ilisema kuwa MCA iliteua Kampuni ya Quntrol, kampuni huru ya ukaguzi na upimaji wa dawa iliyoko Mumbai, kutoa Ripoti a Ukaguzi na Uchambuzi (CRIA) kuidhinisha usafirishaji wote kutoka India.

"Quntrol itafanya uhakiki wa hati, ukaguzi halisi wa shehena na sampuli, kwa uchunguzi wa kimaabara kwa kila shehena," barua hiyo ilisema.

"Ikiwa ulinganifu utathibitishwa katika viwango vyote, Quntrol itatoa hati ya lazima ya CRIA. Ikiwa ulinganifu hautathibitishwa kuhusiana na ubora wa bidhaa, usafirishaji utawekwa karantini au kukamatwa na MCA na hatua muhimu za udhibiti zitachukuliwa."

Janneh Kaira aliiambia Reuters sheria hiyo "inatumika kwa India kwa sasa pekee". Tangu Juni 1, India imefanya vipimo kuwa vya lazima kwa dawa zote za kikohozi kabla hazijasafirishwa nje ya nchi.

Raghuvanshi hakujibu ombi la Reuters la kutoa maoni. Katika barua kwa wasimamizi wa majimbo ya India, aliwataka kuzingatia miongozo mipya ya Gambia.

"Hii ni kwa taarifa yako na hatua za haraka," Raghuvanshi alisema katika barua iliyotumwa kwa tovuti ya Shirika Kuu la Kudhibiti dawa nchini India Jumatano.

Ikiwa na watu milioni 2.5, Gambia ni mojawapo ya nchi ndogo na maskini zaidi barani Afrika. Benki ya Dunia inafadhili maabara ya majaribio nchini Gambia lakini bado haijakamilika.

Barua hiyo ilisema Quntrol itatuma sampuli za majaribio kwa "moja ya maabara ya uchambuzi iliyoidhinishwa na MCA". Haikusema ikiwa maabara hiyo itakuwa nchini India au kwingineko.

Takriban watoto 70, wengi wao wakiwa chini ya umri wa miaka 5, walifariki nchini Gambia mwaka jana kutokana na madhara figo ambayo madaktari wamehusisha na dawa mbovu za kikohozi kutoka India.

Shirika la afya duniani lilisema mwaka jana kwamba dawa za kikohozi zilizotengenezwa India zilikuwa na sumu hatari ya ethylene glikoli na diethylene glikoli - ambayo hutumiwa kwa kawaida katika maji ya breki za gari na bidhaa zingine ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu.

Viungo hivi vinaweza kutumiwa na watendaji wasio waaminifu kama mbadala kwa propylene glikoli, ambayo ni msingi mkuu wa dawa za sharubati - kwa sababu zinaweza kugharimu chini ya nusu ya bei - wanasema wataalam wa utengenezaji.

TRT World