Waziri wa wa nchi wa Madini wa Ethiopia Million Mathews.| Picha: Shirika la habari la FANA

Makampuni ambayo yamekuwa yakijishughulisha na utafiti na uzalishaji wa madini huko Tigray yataanza kufanya kazi hivi karibuni - Wizara ya Madini.

Wizara ya nchi ya Madini nchini Ethiopia imetangaza kuweka mikakati ya kurejesha shughuli za kuzalisha madini katika eneo la Tigray hivi karibuni ili kuyawezesha makampuni ambayo yamekuwa yakitafiti na kuchimba madini mbalimbali yakiwemo dhahabu katika eneo la Tigray kuendelea na kazi zao.

Waziri wa nchi wa Madini Million Mathews amefafanua kuwa hapo awali kampuni za kimataifa zilizokuwa zikiendesha uchunguzi na uchimbaji madini katika eneo hilo la Tigray, zimekuwa zikipata shida katika utekelezaji kazi zao kutokana na changamoto za awali.

Hata hivyo, Waziri Mathews amesema kuwa baadhi ya shughuli za uchimbaji zinaweza kuanza kazi sasa.

Mathews ameeleza kuwa, mkataba wa amani wa Pretoria uliosainiwa mwaka jana baina ya serikali ya Ethiopia na TPLF, ili kusitisha mapigano, na kuleta amani ya kudumu, umeleta nafuu kwa wadau husika na sekta ya madini nchini humo kwa jumla.

Utulivu wa kudumu, umefanikisha mazingira mazuri iliyopelekea makampuni yanayoshiriki katika uzalishaji na utafutaji wa dhahabu, saruji na madini mengine katika eneo la Tigray kurejea kazini.

Waziri wa nchi aliongeza kuwa tayari kiwanda cha saruji cha Mesbo kilichopo mkoani Tigray kimeanza kufanya kazi huku akiongeza kuwa wengine kampuni zingine tayari zimeanza harakati za kurejea kuanza kazi.

Mathews ametaja kuwa tayari Benki ya Dhahabu iliyofungwa, imefunguliwa tena na wataalamu wamepewa kibali cha kuanza mfumo wa ununuzi wa dhahabu huku akiongeza kuwa wanashirikiana na utawala wa mpito wa Ukanda wa Tigray ili kufufua uwezo wa uzalishaji wa sekta hiyo.

Waziri huyo wa nchi pia alisema uongozi mpya wa mpito wa Tigray umewachukulia hatua kali waliokuwa wakiingia na kuzalisha madini kiholela kinyume cha sheria. Amesifu kuwa hatua hii itawawezesha wachimbaji halali wenye leseni na vyama vya uchunguzi kuanza kufanya kazi kwa kujiamini.

Aidha, shirika la ESA liliripoti kuwa makampuni mengine ya kimataifa ya uchimbaji madini, ikiwa ni pamoja na Kampuni ya Newmont, maarufu katika sekta ya madini ya dhahabu duniani, yamethibitisha kuwa yataanza tena shughuli zao katika eneo hilo hivi karibuni.

Waziri huyo wa nchi alikamilisha kwa kusema wizara ya madini itatoa msaada wote unaohitajika kwa makampuni hayo kwani sekta ya madini ina mchango mkubwa kwa taswira ya nchi na ufufuaji wa sekta hiyo.

TRT Afrika