Kupitia mtandao wa Twitter bilionea Ellon Musk anaendelea kutoa taarifa mpya juu ya nani hasa anastahili kuwekewa tiki ya bluu kwenye ukurasa wake kuanzia mwezi April.
"Ukurasa wowote wa Twitter ambao unahusiana na taasisi iliyo idhinishwa moja kwa moja utawekewa tiki ya blue" ameandika Elon Musk
Kwa mujibu wa tovuti rasmi ya mtandao wa Twitter, taasisi ambazo tayari zimeidhinishwa zinaweza kupendekeza mtu mmoja mmoja au kampuni inayohusiana nao ili wapate kuidhinishwa.
Kwa mfano watu hao ni viongozi, watu wanaoendesha kurasa za taasisi, waajiriwa wa kampuni husika au makampuni.
Watumiaji hao watawekewa mmoja ya tiki ya twiter yenye rangiinayoambatana na
Watumiaji waliounganishwa watapokea moja ya beji za uthibitishaji zenye msimbo wa rangi za Twitter pamoja na "beji ya washirika," iliyoambatana na picha ndogo ya wasifu wa kampuni mama ambayo itawapeleka watumiaji moja kwa moja kwa shirika linalo shirikiana ikiwa mtu atabofya, Twitter imethibitisha
Ingawa mashirika yanaweza kuteua washirika wengi wanavyotaka, kumbuka kila mtumiaji atawagharimu dola $50 zaidi kila mwezi ukijumuisha na ada ya usajili ya Mashirika Yaliyoidhinishwa ya dola $1,000 kila mwezi, bila kodi.
Watumiaji wakujitegemea ambao hawajaunganishwa na shirika lililo tayari kuwaorodhesha kama mshirika wanaweza kupata tiki yao ya uthibitishaji kwa kununua usajili wao wa tiki ya bluu ya Twitter kwa dola $8 kwa mwezi au dola $84 kwa mwaka.
Je upatayari kulipa dola 8 za kimarekani kila mwezi ili kupata tiki ya blue ya mtandao wa Twitter.