PICHA YA AWALI: Waislamu wa Kongo waliohamishwa wakiwa kwenye makazi ya muda katika kambi ya Mugunga ilioko nje ya Goma / Picha: Reuters

Mazishi ya waathirika wa mashambulizi ya bomu katika kambi ya wakimbizi ya Mugunga yameahirishwa hadi Jumatano kusubiri ujenzi wa makaburi kukamilika.

Awali, raia hao wafikao 35, walipangwa kuzikwa siku ya Jumapili, Mei 12, 2024.

Makombora kadhaa yalilenga kambi ya wakimbizi ya Mugunga, Goma, Mei 3.

Mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya watu 14 hapo awali na majeraha makubwa lakini idadi ya watu waliouawa iliongezeka hadi 35.

Ingawa hakuna kundi lolote limedai kutekeleza uvamizi uliowaua watu 35, inashukiwa kuwa lilifanywa na makundi ya waasi.

DRC inashutumu Rwanda kwa kujaribu kunyakua ardhi yake yenye madini, na kuunga mkono waasi wa M23, lakini Rwanda imekanusha madai hayo.

TRT Afrika na mashirika ya habari