IOM inasema kuwa Idadi hiyo kubwa inatokana hasa na wimbi jipya la mapigano Mashariki mwa DRC./ Picha: Reuters 

Na Ramadhan Kibuga

TRT Afrika, Bujumbura, Burundi

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM, limeonya kulipuka kwa idadi ya wakimbizi wa ndani nhini Sudan kufikia takriban milioni 7, ikiwa ndio idadi kubwa zaidi kuwahi kutokea.

IOM inasema kuwa Idadi hiyo kubwa inatokana hasa na wimbi jipya la mapigano Mashariki mwa DRC.

Pia iliongeza kuwa asilimia kubwa ya wakimbizi hao wa ndani wanahitaji msaada wa kibinadaamu wa dharura.

Hii ni mojawapo ya migogoro mikubwa ya wakimbizi wa ndani na janga la kibinadamu ambalo Shirika la Kimataifa la Uhamiaji litajaaribu kutafutia ufumbuzi.

Shirika la IOM limeongeza juhudi za kuwasaidia wakimbizi hao wa ndani, ambao idadi kubwa wanapatikana katika mikoa ya Mashariki: Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, Ituri na Tanganyika.

Sehemu kubwa ya Mashariki mwa Congo inashuhudia migogoro ya kivita kwa zaidi ya miongo mitatu.

Hali imekuwa mbaya zaidi baada ya kuibuka upya tena kundi la waasi la M23 mwishoni mwa mwaka wa 2021.

Katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini pekee, zaidi ya watu Milioni 1 wametoroka makaazi yao kutokana na mapigano.

Mapigano hayo yameongezeka hasa kuanzia mwanzoni mwa mwezi huu wa Oktoba Kaskazini mwa Goma kati ya Jeshi la Congo, Waasi wa M23 na Makundi mengine yenye silaha.

Shirika la IOM limetoa wito wa msaada wa haraka hasa kwa wale wanaohitaji zaidi ikiwemo kinamama na watoto ambao wamesongamana katika kambi za wakimbizi wa ndani bil amahitaji y amsingi ya maisha.

TRT Afrika