Nigeria wamepanda jedwali katika kundi lao kufuatia uamuzi huu wa CAF / Picha: Ukurasa wa X - NFF

Shirikisho la Soka barani Afrika limetangaza kuwa Shirikisho la Soka la Libya lilikiuka kanuni muhimu kuhusu mechi yao ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Nigeria.

LFF ilibainika kukiuka Kifungu cha 31 cha Kanuni za AFCON, pamoja na Kifungu cha 82 na 151 cha Kanuni za Nidhamu za CAF. Ukiukaji huu unahusiana na viwango vya shirika na maadili vilivyowekwa kwa mashindano ya kimataifa ya kandanda chini ya mamlaka ya CAF.

''Mechi nambari 87 , Libya v Nigeria katika shindano ya Total Energies la kufuzu taifa bingwa Afrika 2025 (iliyoratibiwa kuchezwa 15 Ooktoba mjini Benghazi) imetangazwa kuhsindwa kwa Libya kwa mabao 3-0.'' ilisema taarifa ya CAF.

Nigeria na libywa waliingia katika mzozo baada ya timu ya Nigeria kuachwa wakihangaika waliposafiri Libya, ambapo ndege yao ililazimishw akutua uwonja wa mbali na kukosa kuhudumiwa kwa saa nyingi.

Timu ya Nigeria ilichukua hatua kurudi nyumbani bil akucheza mechi hiyo waliodai kuwa walikuwa wanafanyiwa hiana na Walibya.

Hata hivyo Libya ililalamika kwa Shirikisho la soka CAF kuwa huo ni utovu wa nidhamu upande wa Nigeria kwani makosa yalitokea sio kwa kusudi, n awakaomba Nigeria kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Lakini mamboi yamewageukia kwani adhabu wamepokea wao Libya.

''Shirikisho la soka la Libya limeamrishwa kulipa faini ya dola 50,000 ndani ya siku 60 tangu kupokea agizo hili'' iliendelea kusema taarifa hiyo.

Pia katika hukumu yake CAF imesema kuwa uamuzi huu unafuta maombi mengine yote ya msamaha au kupunguziwa adhabu.

TRT Afrika