PICHA YA AWALI: Kiongozi wa mpito wa Burkina Faso Ibrahim Traore, akiwa na wenzake, viongozi wa Mali, na Niger, Muungano wa Sahel, walipokutana Niamey / Picha: Reuters

Watu kadhaa wakiwemo raia wameuawa katika shambulio la wanamgambo nchini Burkina Faso, vyanzo vya ndani na vya usalama viliiambia AFP.

Kulingana na mkazi mmoja wa eneo hilo, walikuwa "vijana, ambao walijitokeza kwa idadi kubwa kusaidia askari kuchimba mitaro kuzunguka mji, kujikinga na mashambulio yanayowezekana na makundi ya kigaidi yenye silaha".

Wanamgambo wanaoshirikiana na Al-Qaeda na Kundi la Daesh wameanzisha uasi mkubwa nchini Burkina Faso tangu 2015 na kuwaua maelfu na kuwalazimu watu milioni mbili kuhama.

Shambulio la hivi karibuni lilitekelezwa na watu waliojihami kwa silaha katika kijiji cha Barsalogho Kaskazini ya Kati mwa Burkina Faso Jumamosi, vyanzo mbalimbali vilisema.

Akishutumu" shambulio la woga na la kinyama," Waziri wa Mawasiliano Rimtalba Jean Emmanuel Ouedraogo alisema lilifanywa na "makundi ya wahalifu."

Kwa upande wake, Waziri wa Usalama Mahamadou Sana amesema kuwa raia waliuawa katika shambulio hilo, licha ya "jibu na msaada wa anga."

Wanamgambo hao waliwalenga "wanawake, watoto, wazee, wanaume, bila kubagua," Ouedraogo alisema kwenye kituo cha televisheni cha kitaifa.

Afisa mmoja wa usalama ambaye aliomba kutotajwa alisema kulikuwa na "watu kadhaa waliokufa" wakiwemo raia na vikosi vya usalama.

Wengi wa "majeruhi" walipelekwa hospitalini katika mji mkuu wa Mkoa wa Kaya, umbali wa kilomita 45 (maili 28), chanzo kiliongeza.

Baada ya kuchukua madaraka katika mapinduzi mnamo Septemba 2022, viongozi Wa Mapinduzi ya Burkina waliwafukuza wanajeshi na wanadiplomasia kutoka mtawala wa zamani wa kikoloni, Ufaransa, na kugeukia Urusi kwa msaada wa kijeshi.

AFP