| Swahili
AFRIKA
1 DK KUSOMA
Burkina Faso: 15 wauawa katika shambulio la kanisa
Takriban watu 15 wamethibitishwa kufariki katika shambulizi la kutumia silaha kwenye kanisa moja kaskazini mwa Burkina Faso.
Burkina Faso: 15 wauawa katika shambulio la kanisa
Maafisa wa kanisa nchini Burkina Faso wameelezea tukio la Februari 25, 2024 kama shambulio la "kigaidi". / Picha: AP / Others
26 Februari 2024

Takriban raia 15 waliuawa na wengine wawili kujeruhiwa wakati wa shambulio la "kigaidi" dhidi ya kanisa la Kikatoliki wakati wa misa ya Jumapili kaskazini mwa Burkina Faso, afisa mkuu wa kanisa hilo alisema.

"Tunakufahamisha juu ya shambulio la kigaidi ambalo jumuiya ya Kikatoliki ya kijiji cha Essakane ilikumbwa nalo leo, Februari 25, walipokuwa wamekusanyika kwa ajili ya sala ya Jumapili," kasisi wa Dayosisi ya Dori, Jean-Pierre Sawadogo, alisema katika taarifa yake aliyotuma kwa shirika la AFP.

Idadi iliyotolewa ya awali ni vifo 15, wawili walijeruhiwa, aliongeza.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika