Wanachama wa BRICS

Upanuzi wa BRICS ulitawala majadiliano wa mkutano wa BRICS, mjini Johannesburg, Afrika Kusini huku kati ya angalau nchi 20 hadi 40 kutoka sehemu tofauti duniani zikisaka uanachama ili kujiunga na Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini kwenye muungano.

Hata hivyo, uvumi huo ulifika kileleni siku ya Alhamisi, wakati mwenyeji, Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, alipotangaza kwamba BRICS imeialika rasmi nchi sita kujiunga na umoja huo: Saudi Arabia, Iran, UAE, Argentina, Misri na Ethiopia.

Kwa muda mrefu, BRICS imekuwa ikitajwa kama chombo chenye uwezo wa kubadilisha mchezo ambacho kinaweza kuleta mpangilio mpya wa kimataifa, unaotegemea mgawanyo wa haki na usawa zaidi wa mamlaka na ushirikiano wa pande nyingi.

Ujumbe huo huo ulikaririwa katika mkutano wa kilele wa mwaka huu na viongozi wote, na kujumuishwa kwa wanachama sita wapya kunatoa uthibitisho zaidi kwa lengo lililotajwa la kambi hiyo.

Hata hivyo, wachambuzi wanaamini kuwa mwelekeo wa mabadiliko ya kweli bado inajaa changamoto kubwa.

"Ulimwengu unataka utaratibu mpya, lakini hautakuja bila maumivu, machozi na upinzani kutoka kwa wale ambao walikuwa wakitawala katika mpangilio uliopita," Lesiba Teffo, mchambuzi wa kisiasa nchini Afrika Kusini, aliiambia Anadolu.

Alisema kundi la BRICS linalenga kuunda utaratibu wa kimataifa usiozingatia dola, Marekani na Magharibi kwa upana zaidi.

Kwenye tathmini ya Teffo, mazingira ya sasa ya kimataifa inafanya lengo hilo kufikiwa zaidi, hasa kutokana na ukubwa wa maslahi katika uanachama kutoka nchi duniani kote.

"Inaenda kuonyesha kuwa BRICS inakua katika umuhimu wake, kimo chake na pia katika ushawishi wake duniani," aliongeza.

"Inaenda kuonyesha kuwa BRICS inakua katika umuhimu wake, kimo chake na pia katika ushawishi wake duniani," alisema.

Msukumo kutoka Magharibi

Teffo anasisitiza kuwa suala lolote linalohusiana haswa na upanuzi wa BRICS, litapingwa na mababe wa Magharibi ambao wametawala dunia kwa karne nyingi.

"Tusijifanye kuwa nchi za Magharibi hazitafanya kila liwezalo kufanya hali iwe vigumu, au hata isiwezekane, kuzuia ufanisi wa BRICS," alisema.

Teffo alitumia mfano wa kutokuwepo kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin katika mkutano wa kilele wa Johannesburg, na badala yake kuwakilishwa na Waziri wake wa Mambo ya Nje Sergey Lavrov.

Putin, ambaye alihutubia mkutano huo kwa njia ya video, hakufika Afrika Kusini kwa sababu ya kibali cha kukamatwa kwake kilichotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuhusu madai ya uhalifu wa kivita nchini Ukraine.

Putin, ambaye alihutubia mkutano huo kwa njia ya video, hakufika Afrika Kusini kwa sababu ya kibali cha kukamatwa kwake kilichotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuhusu madai ya uhalifu wa kivita nchini Ukraine.

Afrika Kusini ni mwanachama wa ICC na ingetarajiwa kumkamata Putin, jambo ambalo ilisita kufanya kwani Rais Ramaphosa alisema ingeleta hatari ya vita kati yake na Urusi.

Teffo alisema hasira juu ya uwezekano wa kuhudhuria kwa Putin ilichochewa na nchi nyingi za Magharibi ambazo hata sio watia saini wa ICC, akimaanisha Amerika. Nchi za Magharibi zilikuwa zikiishinikiza Afrika Kusini kumkamata Putin iwapo angeingia nchini humo na hii ililenga kuleta mgawanyiko ndani ya umoja huo, alieleza.

Teffo alisema hasira juu ya kuhudhuria kwa Putin ilichochewa na nchi nyingi za Magharibi ambazo hata sio watia saini wa ICC, kama vile Marekani.

Nchi za Magharibi ziliishinikiza Afrika Kusini kumkamata Putin iwapo angeingia nchini humo na hii ililenga kuleta mgawanyiko ndani ya umoja huo, alieleza.

Kinyang’anyiro kipya cha Afrika’

Hata hivyo, licha ya shangwe na umakini, hakuna uwezekano wa BRICS kuunda aina yoyote ya mpangilio mpya wa ulimwengu, kulingana na Ahmed Jazbhay, profesa wa siasa katika Chuo Kikuu cha Afrika Kusini.

"BRICS inasaka tu mpangilio mpya wa dunia ili iweze kupata kiti mezani," aliiambia Anadolu.

"Iwapo itakuwa yenye usawa, na haki kwa nchi zote duniani au kama italegeza minyororo ya ukoloni mamboleo, kwa maoni yangu, haijabainika. BRICS na mipango yake pia inaweza kuonekana kama "kinyang'anyiro kipya kwa Afrika."

Nchi nyingi zinazopinga utawala wa kimataifa wa Amerika, kama vile Uchina na Urusi, nazo zinalenga tu nchi za Kiafrika, alielezea.

Kwa Jazbhay, BRICS sio "kundi la kupinga ubeberu linalodai kuwa."

"Inaomba tu kiti kwenye meza na ugawaji upya wa usawa zaidi wa mpangilio wa ulimwengu wa sasa, ambao kimsingi umewekwa upya," alisisitiza.

Alisema mataifa ya Afrika lazima "yawe makini na mataifa hayo na kutoegemea upande wowote," akisisitiza kwamba wasitarajie haki na usawa "kutoka kwa nchi kama Urusi, India na Uchina ambazo zinaongozwa na wababe."

AA