Mwanasiasa wa Uganda Bobi Wine amesema kuwa atagombea kiti cha Urais katika uchaguzi utakaofanyika Januari 12, 2026.
Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 42, ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, ameweka wazi azma yake katika mahojiano yake na gazeti la Monitor la Uganda, siku ya Jumapili.
Katika uchaguzi wa mwaka 2021, Rais Yoweri Museveni kutoka chama National Resistance Movement (NRM) alipata asilimia zaidi ya 58 ya kura huku Bobi Wine wa chama National Unity Platform (NUP), akipata asilimia zaidi ya 35 ya kura zote zilizopigwa.
Hata hivyo, chama cha Bobi Wine kimekana tuhuma za Rais Museveni.
Kiongozi wa upinzani bungeni nchini humo Joel Ssenyonyi, ambaye pia ni mwanachama wa NUP amesema kuwa Rais Museveni alikuwa na hofu na namna vijana walivyokuwa na wanavutiwa na vuguvugu la NUP.
'Utulivu na uendelevu'
Hata hivyo, Rais Museveni, mwenye umri wa miaka 80, amesema kuwa uongozi wake unatoa uhakika wa uendelevu na utulivu.
Kwa upande wake, Wine, anasema kuwa kizazi kikubwa cha Uganda kinataka "kuona mabadiliko."