Watumiaji wa Petroli nchini Tanzania watalazimika kulipia zaidi huduma hiyo kufuatia ongezeko la bei la bidhaa hiyo.
Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa Aprili 1, 2024, EWURA imesema kupanda kwa gharama za bidhaa hiyo kumechangiwa na ongezeko la bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia kwa wastani wa asilimia 3.90 kwa mafuta ya petroli na kupungua kwa wastani wa asilimia 1.31 kwa mafuta ya dizeli.
Kiwango hicho cha bei ni cha juu zaidi tangu shilingi 3, 410 (dola 1.32) iliyotangazwa Agosti, 2022.
Kwa mujibu wa EWURA, mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Mei 2024, yamechangiwa na ongezeko la bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia kwa wastani wa asilimia 3.90 kwa mafuta ya petrol na kupungua kwa wastani wa asilimia 1.31 kwa mafuta ya dizeli.
Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko huku mamlaka hiyo ikihamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.
Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani isipokuwa bei hizo zisizidi bei kikomo au kuwa chini ya bei iliyoruhusiwa, mamlaka hiyo imeagiza.
Pia imevitaka vituo vyote vya mafuta kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana yakionesha bei za mafuta, punguzo, vivutio vya kibiashara vinavyotolewa na kituo husika.