Kenya imefuzu kwa mara ya kwanza kabisa katika ligi ya Basketiboli ya Bara Afrika BAL / Picha :  @roadtoBAL

Timu ya Nairobi City Thunders kutoka Kenya wamevishwa kirauni kama mabingwa wa divisheni ya Mashariki baada ya kuwapiga Kriol ya Cape Verde 99-86 katika fainali jijini Nairobi.

Mechi ya Jumanne usiku katik w a Kasarani ilikuwa kutafuta sifa ya ubabe wa eneo la Mashariki kwani tayari timu zote mbili zilikuwa zimeshajipatia walichokuwa wanatafuta, ambayo ni kufuzu kwa ligi ya Afrika ya basketboli 2025 , BAL.

Kenya ilifuzu Jumatatu baada ya kuilaza Uganda City Oilers ambao wanakosa kwa mara ya kwanza katika miaka minne katika shindano hilo, huku kwa Kenya ikiwa mara yao ya kwanza kufuzu.

Unachotakiwa kujua juu ya ligi ya BAL

Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika (BAL) ni ligi ya kitaalamu ya mpira wa vikapu barani Afrika, iliyoandaliwa na NBA na FIBA.

Awamu ya tano ya ligi hiyo itachezwa kati ya 5 Aprili hadi 14 Juni mwaka 2025 kati ya timu 12 za kitaalamu, ambapo timu saba zilifuzu moja kwa moja kama mabingwa wa kitaifa na tano zinafuzu kwa ubingwa wa kikanda kama walivyofuzu Nairobi City Thunder.

Fainali ya michuano hiyo itafanyika Juni 14 kwenye Uwanja wa SunBet Arena mjini Pretoria, ikiwa ni mara ya kwanza Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa Fainali za BAL.

TRT Afrika