Uingereza itatafuta uungwaji mkono kutoka kwa wanachama wengine wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu kwa matakwa yake ya kutaka pande zinazozozana nchini Sudan zisitishe uhasama na kuruhusu utoaji wa misaada, wizara ya mambo ya nje ya Uingereza ilisema.
Huku London ikishikilia urais wa zamu wa baraza hilo, waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Lammy anatazamiwa kuongoza kura kuhusu rasimu ya azimio lililopendekezwa na Uingereza/Sierra Leone, ambalo pia linatoa wito wa kulindwa kwa raia.
Lammy atasema "Uingereza kamwe haitaiacha Sudan kusahauliwa" na kutangaza kuongeza mara mbili msaada wa Uingereza hadi pauni milioni 226 ($285 milioni), kulingana na taarifa kutoka kwa wizara yake.
Mgogoro wa kuwania madaraka kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka wa kijeshi ulianza mwezi Aprili 2023 kabla ya mpango wa mpito kuelekea utawala wa kiraia, na kuua maelfu ya watu na kusababisha mzozo mkubwa zaidi wa watu kuhama makaazi duniani.
Wizara hiyo ilisema Lammy pia atakikosoa vikwazo vya Israel dhidi ya misaada ya wa kibinadamu huko Gaza na kutoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano pamoja na kuachiliwa kwa mateka wote.
Kuhusu vita vya Ukraine, alipaswa kusema kwamba Uingereza "itasimama na Ukraine hadi hali halisi itakapopambazuka huko Moscow".