Dkt Saulos Chiima, aliyekuwa Makamu wa Rais wa Malawi. 

Baraza la Taifa la Michezo nchini Malawi limesimamisha michezo yote kwa muda kufuatia kifo cha makamu wa rais wa nchi hiyo Dkt Saulos Chilima na viongozi wengine tisa.

Kuahirishwa kwa shughuli za michezo kunaenda sambamba na tangazo la Rais Dkt Lazarus Chakwera la siku 21 za maombolezo.

Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Chilima alikuwa mdau mkubwa wa michezo. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mtendaji Mkuu wa Bazara hili, Henry Kamata, kusitishwa kwa muda kwa shughuli za michezo, kunatoa fursa kwa jamii ya wanamichezo kuungana na Rais Chakwera na taifa kwa ujumla kutika kuomboleza kifo cha makamu wa rais na viongozi wengine.

Itakumbukwa kuwa, Makamu wa Rais alikuwa mchezaji mzuri wa gofu na mpira wa kikapu.

Pia atakumbukwa kwa mchango wake katika sekta ya michezo, akiwa kama mwenyekiti wa michango ya Kombe la FAM mwaka 2005 na vile vile mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya FAM 2007, ambapo alikuwa na mchango mkubwa wa kupata ufadhili wa Kombe la Standard Bank.

TRT Afrika