| Swahili
AFRIKA
1 DK KUSOMA
Ajali ya treni yajeruhi watu 70 nchini Tanzania
Ajali hiyo imetokea katika eneo la Stesheni ya Kazuramimba iliyoko mkoani Kigoma, baada ya mabehewa sita kuacha njia na kuanguka.
Ajali ya treni yajeruhi watu 70 nchini Tanzania
Ajali hiyo imetokea baada ya mabehewa  sita kati ya 12 ya treni hiyo kuacha njia na kupinduka./Picha: Wengine / Others
28 Agosti 2024

Watu 70 wamejeruhiwa nchini Tanzania kufuatia ajali iliyohusisha mabehewa 12 ya treni inayomilikiwa na Shirika la Reli la nchi hiyo (TRC).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika hilo, ajali hiyo ilitokea Agosti 28, kati ya Shesheni ya Kazuramimba na Uvinza mkoani Kigoma.

Kulingana na TRC, ajali hiyo imetokea baada ya mabehewa sita ya treni hiyo kuacha njia na kusababisha watu 70 kujeruhiwa.

TRC imesema kuwa hali za majeruhi hao zinaendelea vizuri huku, majeruhi 57 wakiwa wameruhusiwa.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika