Kuzungumza juu ya uhifadhi wa mazingira sio tu nchini Kenya lakini kote Afrika, ni ngumu bila kumtaja marehemu mkenya Profesa Wangari Maathai, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel. Alikuwa kiongozi shupavu katika siasa ambaye aliitetea mazingira nchini Kenya na Afrika kote, akaacha historia ya kudumu katika maisha yake.
Idadi ya watu wa afrika, biashara, na mifumo ikolojia inaathiriwa sana na mambo yanayosababishwa na mabadiliko ya hali ya anaga kama vile ukame na mafuriko makubwa. Kuna mabadiliko katika mifumo ya mvua, barafu inayeyuka, na maziwa muhimu yanapungua.
Taasisi ya Rasilimali Duniani (WRI) ilitunukiwa dola milioni 100 na shirika lisilo la kiserikali(NGO) ya TED huko Vancouver, Canada.
''Nina furaha isiyo kifani kuwa Restore Local imechaguliwa kwa ufadhili huu,hii ni ishara tosha ya imani kutoka kwa mashirika ya kitaifa katika mambo yanayoongozwa na wenyeji wa Afrika," alisema Bi. Mathai wakati akipokea ruzuku hio
Wanjira Mathai, bintiye marehemu mwanamazingira Prof. Wangari Mathai, anaendeleza urithi wa mama yake kwa kuendelea kuongoza kama makamu mkurugenzi wa kanda ya Afrika katika Taasisi hii.
Pesa hizi zitasaidia kuharakisha urejeshaji wa ardhi unaoongozwa na wenyeji katika mandhari ya Afrika. NGO TED, shirika lisilo la faida kupitia 'Audacious Project' yake, mpango shirikishi wa ufadhili uliozinduliwa mwaka wa 2018.
"Kurejesha ardhi iliyoharibiwa kunaweza kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya anga na kulinda jamii kutokana na athari zake mbaya zaidi. Inaweza pia kurejesha uzalishaji, kuunda ajira na kuboresha mapato ya kila mtu." alisema Wanjira.
Anananuia kuléta miradi mbali mbali itakayosaidia katika kupunguza athari za mabadiliko ya anga kwa kijamii mbali mbali kwa kiwango kikubwa, ikitafuta kuhakikisha mazingira yanayofaa kwa wote.
Wanjira anasema sasa yuko tayari kuongoza mradi mpya huo wa kurejesha ardhi katika Ukanda wa Kakao wa Ghana, Bonde la Ufa, Ziwa Kivu, na Bonde la Mto Rusizi kwenye mpaka wa DRC-Rwanda-na Burundi.
Ana matumaini kwamba kwa kuharakisha kampeni ya AFR100, mradi wa kurejesha hekta milioni 100 za ardhi iliyoharibiwa barani Afrika ifikapo 2030 Afrika itawezekana iwapo Afrika itaendelea kupiga hatua mbele na kafuata mwelekeo sahihi.
Wakulima wa ndani, wamiliki wa biashara, na kila mmoja ana uwezo wa kukarabati kabisa ardhi iliyoharibiwa ya Afrika, anadai Bi Maathai, hata wakati wataalam wa Afrika wanaendelea kuzungumza kwa sauti kubwa zaidi kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.