Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki, Deng Alor Kuol akijiandaa kuwasilisha bajeti ya Jumuiya hiyo kwa mwaka wa fedha 2024.2025./Picha: EALA X

Na Edward Qorro

TRT Afrika, Istanbul, Uturuki

Nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimeazimia kuimarisha amani ya kikanda baada ya kuwasilisha bajeti ya dola milioni 112, Juni 25, 2024, jijini Arusha nchini Tanzania.

Jumuiya hiyo, yenye nchi wanachama 8, pia imelenga kuimarisha uwekezaji na biashara ya kikanda kupitia bajeti hiyo, wakati wa mkutano wa 4 wa kikao cha pili cha bunge la tano la EALA.

Mara baada ya wasilisho la bajeti hiyo na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Afrika Mashariki kutoka Sudan Kusini Deng Alor Kuol, wabunge 63, kutoka nchi wanachama watapata siku mbili za kuisoma na kuijadili bajeti hiyo.

Jumuiya hiyo, yenye nchi wanachama 8, pia imelenga kuimarisha uwekezaji na biashara ya kikanda kupitia bajeti hiyo, wakati wa mkutano wa 4 wa kikao cha pili cha bunge la tano la EALA./Picha: EALA X

Bajeti hiyo, pia itaangazia uanzishwaji wa taasisi za fedha kuelekea mchakato muhimu wa kuwa na sarafu ya pamoja.

Kulingana na Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki, dola milioni 67.7 ni vyanzo vya ndani kutoka nchi wanachama wakati dola milioni 43.9, inahusisha michango kutoka washirika wa maendeleo.

Katika mwaka wa fedha uliopita, EALA ilipitisha bajeti ya dola milioni 103.8, katika kufanikisha shughuli mbalimbali za Jumuiya hiyo, yenye makao yake makuu jijini Arusha nchini Tanzania.

"Wakati Tanzania, Kenya na Uganda zinawasilisha michango yao asilimia 100, bado nchi zingine zinasuasua kufikia malengo hayo," amesema James Millya, mjumbe kutoka Tanzania.

Kulingana na Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki, dola milioni 67.7 ni vyanzo vya ndani kutoka nchi wanachama wakati dola milioni 43.9, inahusisha michango kutoka washirika wa maendeleo./Picha: EALA X

Mwenendo usioridhisha wa nchi wananchama kuwasilisha michango yao kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki imekuwa ni kilio cha muda mrefu kwa sasa.

Baadhi ya wabunge wa EALA, wanaharakati na watu kutoka kada mbalimbali wametaka nchi zinazishindwa kutimiza sharti hilo la kisheria, kulingana na mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo.

TRT Afrika