Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza Mei 29 kuwa siku ya uchaguzi mkuu ujao nchini humo.
Wapiga kura watachagua Bunge jipya la Kitaifa pamoja na bunge la mkoa katika majimbo yote tisa nchini. Bunge humchagua rais baada ya kura.
"Rais Ramaphosa anatoa wito kwa wapiga kura wote wanaostahiki kushiriki kikamilifu katika hatua hii muhimu na ya kihistoria ya kalenda yetu ya kidemokrasia," taarifa kutoka kwa ofisi ya rais ilisema Jumanne.
Mgao wa umeme, utoaji duni wa huduma na viwango vya juu vya ukosefu wa ajira vinaweza kuumiza chama tawala cha African National Congress (ANC) ambacho Ramaphosa anaongoza.
Ramaphosa atawania muhula wa pili kama rais.
TRT Afrika