| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Simba yamaliza unyonge kwa Yanga
Timu hizo zimekutana tena tangu mara ya mwisho zilipokutana katika mechi ya Ngao ya Jamii, iliyopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani, Zanzibar, Agosti 12, 2026 na Yanga kushinda kwa bao 1-0, la Albert Kangwanda dakika ya 31.
Simba yamaliza unyonge kwa Yanga
Elie Mpanzu wa Simba akimchambua kipa wa Young Africans Djigui Diarra na kufunga bao la pili katika 'Kariakoo Dabi' iliyofanyika Oktoba 10, 2026.

Simba Sports Club ya Tanzania, ilitoka nyuma kwa bao 1 na kupindua matokeo dhidi ya mahasimu wao wa jadi Young Africans, kwa kuifunga 2-1, katika mchezo wa Kariakoo Dabi, uliofanyika Oktoba 10, 2026 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Peter Shalulile aliwatanguliza ‘Wananchi’ katika dakika ya 5 ya mchezo kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Maxi Mpia Nzengeli kabla ya Neo Maema kurudisha bao kwa Simba, katika dakika ya 68 ya mchezo, kabla Elie Mpanzu, kuwaandikia ‘Wekundu wa Msimbazi’ bao la pili katika dakika ya 72.

Timu hizo zimekutana tena tangu mara ya mwisho zilipokutana katika mechi ya Ngao ya Jamii, iliyopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani, Zanzibar, Agosti 12, 2026 na Yanga kushinda kwa bao 1-0, la Albert Kangwanda dakika ya 31.

CHANZO:TRT Afrika Swahili