Uturuki imeadhimisha miaka 103 ya Jamhuri kwa shamrashamra mbalimbali ambazo zimepamba maeneo ya nchi hiyo siku ya Alhamisi.
Bendera za taifa zatamalaki majumbani, maofisini na maeneo ya umma.
Bendera yenye mita 103
Gwaride maalumu lilifanyika katika eneo la Osmancik, ambapo gwaride hilo lilihusisha bendera ya Uturuki yenye mita 103.
Shughuli hiyo, ilitanguliwa na ukimya pamoja na wimbo wa taifa.
Ngoma za jadi zarindima mitaa ya Izmir
Ngoma za kijadi toka kwa wakazi wa Izmir, zilitia nakshi tukio hilo.
Mbio za marathon kwenye daraja la Osmangazi
Kama sehemu ya maadhimisho hayo, mbio maalumu zilifanyika kwenye daraja la Osmangazi huko Kocaeli.
Washiriki wapatao 6,500 kutoka mataifa 19, walishiriki mbio hizo
Waendesha farasi
Sherehe hizo, zilipambwa na waendesha farasi 40 ambao walipita kwenye njia ya kihistoria ya kilomita 95, maarufu kama barabara ya Istiklal.
CHANZO:TRT World and Agencies





















