| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Waziri Mkuu wa Canada kuitembelea Uturuki
Kulingana na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Canada, ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili, hasa katika maeneo ya kiusalama na kiuchumi.
Waziri Mkuu wa Canada kuitembelea Uturuki
Akiwa jijini Ankara, Carney anatarajiwa kuonana na Rais Recep Tayyip Erdogan, ambapo watajadiliana ushirikiano wa nchi zao katika maeneo ya nishati, u

Waziri Mkuu wa Canada, Mark Carney anatarajiwa kuwasili jijini Istanbul akitokea Ankara, katika ziara yake ya kwanza, itakayoanza Oktoba 21 hadi 23.

Kulingana na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Canada, ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili, hasa katika maeneo ya kiusalama na kiuchumi.

Akiwa jijini Ankara, Carney anatarajiwa kuonana na Rais Recep Tayyip Erdogan, ambapo watajadiliana ushirikiano wa nchi zao katika maeneo ya nishati, ulinzi na pia kijamii.

Baada ya kuwasili jijini Istanbul, Carney atakutana na wafanyabiashara na wawekezaji wengine.

Kulingana na ofisi ya Carney, uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili, umekuwa kwa asilimia 50, katika kipindi cha miaka mitano.

Wakati wa ziara yake, Carney anatarajiwa kuangazia fursa za ushirikiano katika nishati, anga za mbali, madini na teknolojia.

Serikali ya Canada imeielezea Uturuki kama mshirika wa kweli wa nchi hiyo.

CHANZO:TRT World and Agencies