| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Naibu mkuu wa polisi wa Afrika Kusini ajiuzulu kufuatia madai ya ufisadi na ngono
Naibu mkuu wa polisi wa Afrika Kusini aliyekuwa amesimamishwa kazi, Shadrack Sibiya, alijiuzulu siku ya Jumatatu huku akikabiliwa na madai ya ufisadi na udhalilishaji wa kingono.
Naibu mkuu wa polisi wa Afrika Kusini ajiuzulu kufuatia madai ya ufisadi na ngono
Shadrack Sibiya alisimamishwa kama naibu mkuu wa polisi wa Afrika Kusini Septemba 2025.

Naibu Mkuu wa polisi wa Afrika Kusini aliyekuwa amesimamishwa kazi, Shadrack Sibiya, amejiuzulu siku ya Jumatatu huku akishtumiwa kwa madai ya ufisadi na udhalilishaji wa kingono.

Sibiya alitakiwa kufika mbele ya kamati ya nidhamu lakini mawakili wake wakawasilisha barua ya kujiuzulu wakati wa kikao hicho, msemaji wa polisi Athlenda Mathe amesema.

“Kutokana na kuwa afisa huyo mwandamizi wa zamani alikuwa anakabiliwa na kesi kuhusu nidhamu yake wakati anajiuzulu, kuondoka kwake polisi hivyo kunafahamika kama kuondoka bila heshima,” Mathe alisema.

Kwa sasa Sibiya yuko gerezani baada ya kukamatwa kwa madai ya ubakaji na kumrubuni mtoto mwezi uliopita. Amekanusha madai hayo. Ombi lake la kutaka aachiwe kwa dhamana limeahirishwa hadi Oktoba 13.

Madai ya ufisadi

Sibiya amekuwa akikabiliwa na uchunguzi kuhusu madai kadhaa ya ufisadi ndani ya polisi nchini Afrika Kusini pamoja na uhusiano na mitandao ya kihalifu katika taifa hilo.

Tume hiyo ya uchunguzi, inayoongozwa na Jaji mstaafu Mbuyiseni Madlanga, inamshtumu Sibiya kwa kupokea fedha nyingi na zawadi kutoka kwa wanaodaiwa kuwa wahalifu.

Wakati wa kutoa ushahidi wake kwa tume, Sibiya alikanusha madai hayo.

Alikuwa amesimamishwa kazi tangu Septemba mwaka uliopita.

 

CHANZO:TRT Afrika Swahili