| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Pakistan, Oman wasema mashambulizi ya Houthi 'hayakubaliki', watoa wito wa kutumika diplomasia
Wakipongeza nafasi ya diplomasia ya Pakistan katika vita vya Marekani kwa Iran, Oman inasisitiza dhamira yake ya kuimarisha ushirikiano wao wa muda mrefu kati ya mataifa hayo mawili.
Pakistan, Oman wasema mashambulizi ya Houthi  'hayakubaliki', watoa wito wa kutumika diplomasia
Wanadiplomasia waandamizi wa Pakistan, Oman watoa wito wa kufanyika kwa majadiliano, diplomasia katika kutatua mizozo kwenye kanda. /Picha: AFP

Wanadiplomasia waandamizi wa Pakistan na Oman wamejadili juhudi za amani katika kanda mjini Islamabad, wakitoa wito wa kufanyika kwa "majadiliano na diplomasia" katika kutatua migogoro kwenye kanda.

Wakihutubia waandishi wa habari kwa pamoja baada ya mazungumzo yao, Ishaq Dar na mwenzake wa Oman, Badr bin Hamad bin Hamood Albusaidi, walisema siku ya Jumatano kuwa wote "kauli yao ni moja", kwa kuwa “ndiyo njia pekee ya ufumbuzi” katika kutatua migogoro kwenye kanda.

Albusaidi aliwasili mjini Islamabad siku ya Jumanne akiwa katika ziara rasmi ya siku mbili huku kukiwa na mzozo mkubwa Mashariki ya Kati kutokana na uhasama kati ya Saudi Arabia na wapiganaji wa Houthi.

Pande zote mbili zilifanya kikao cha nane cha Tume ya Pamoja ya Mawaziri wa Pakistan na Oman.

Dar, katika kauli yake, alisema pande zote mbili zilijadiliana kuhusu mashambulizi ya hivi majuzi ya wapiganaji wa Houthi huko Saudi Arabia, na kuyataja kuwa “hayakubaliki kabisa".

“Nasisitiza kuwa mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu ya raia hayakubaliki. Kaka yangu [Albusaidi] anaunga mkono kauli hii kikamilifu. Ukiukwaji wa sheria ya kimataifa ni hatari kwa amani na usalama katika kanda,” alisema.

“Nasisitiza Pakistan kuunga mkono kikamilifu Saudi Arabia na dhamira yetu ya dhati kwa heshima ya mipaka ya nchi hiyo na usalama kulingana na Makubaliano ya Pamoja ya Ulinzi ya Makkah,” alisema.

Diplomasia kwa lengo la kumaliza vita vya Marekani kwa Iran

Pande zote mbili, alisema kuwa, zilijadiliana kuhusu hali ilivyo katika Ghuba.

Pia alisisitiza kuhusu dhamira ya Pakistan katika kuchangia kimsingi juhudi za kidiplomaisa zenye lengo la kuimarisha amani na usalama katika kanda.

Pia walisisitiza kuhusu kufikishwa bila pingamizi misaada kwa watu wa Gaza.

Katika hotuba yake, Albusaidi alisisitiza kuhusu dhamira ya pamoja ya mataifa hayo mawili kuimarisha ushirikiano kwenye masuala yote ya maslahi ya pamoja

‘‘Sote Oman na Pakistan tunaweka umuhimu mkubwa katika majadiliano na diplomasia kama njia ya msingi ya kutatua changamoto kwenye kanda, kutuliza uhasama na kuimarisha amani na usalama,” alisema.

Wakipongeza nafasi ya diplomasia ya Pakistan katika vita vya Marekani kwa Iran, Oman inasisitiza dhamira yake ya kuimarisha ushirikiano wao wa muda mrefu kati ya mataifa hayo mawili.

Pande zote mbili zilisisitiza uhusiano wao wa karibu na dhamira ya kuimarisha ushirikiano, kulingana na taarifa ya pamoja.

CHANZO:َAA