Raia wa India amepoteza maisha na mwengine kutoka New Zealand kujeruhiwa, baada ya helikopta mbili kugongana wakati zikijaribu kutua katika eneo la Mlima Everest nchini Nepal, siku ya Jumanne.
Helikopta hizo mbili, moja ikimilikiwa na kampuni ya Fishtail Air na nyingine na Air Dynasty, ziligongana wakati wakati zikijaribu kutua katika eneo lililojaa theluji katika wilaya ya Solukhumbu, mapema Jumanne.
ZILIZOPENDEKEZWA
"Raia huyo wa India alipoteza maisha papo hapo,” alieleza Nabin Raja Budhathoko, afisa polisi katika wilaya hiyo.
Kulingana na Budhatoko, majeruhi huyo amehamishiwa Kathmandu kwa matibabu zaidi, huku jitihada zikiendelea kuhamisha mwili wa marehemu kuelekea jiji la Kathmandu.
CHANZO:AFP






















